KARIBU USHIRIKI KUCHANGIA KWA AJILI YA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA
Shule
ya Sekondari Kibaha ni moja ya Shule Kongwe nchini Tanzania. ilianzishwa rasmi
mwaka 1965 na mpaka sasa imeendelea kushika katika nafasi yake ya kuwa
shule ya vijana wenye vipaji maalum.
Shule hii imeweza kutoa wataalaam ambao wamebobea katika fani mbali Serikalini,
katika Mashirika ya Umma, Vyuo vikuu, Taasisi za Kimataifa na Taasisi binafsi.
Mfano
Mzuri ni Raisi Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni
matunda na hazina kubwa kwa Taifa ambayo chimbuko lake ni Shule ya Sekondari
Kibaha.
Kwa
sasa Shule ina zaidi ya miaka hamsini, hivyo ni dhahiri miundo mbinu yake
inahitaji ukarabati mkubwa ili irejee kuwa na sura ya awali.
Ukiwa
ni Mwanafunzi uliyesoma katika Shule hii, mdau katika Elimu, Mfanyabiashara,
Mzazi na wote wenye mapenzi mema ya kuendeleza Elimu kwa vijana mnakaribishwa
kuchangia katika mfuko maalum wa ukarabati wa shule hii.
Kwa
mawasiliano zaidi wasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Asumpter Mshama
ambaye ndiye Mhamasishaji ukarabati wa Shule ya Sekondari Kibaha na Bw. Robert Shilingi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha
No comments: