WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA KULETA MABADILIKO KATIKA UJASIRIAMALI KWA JAMII
Tarehe: 28 Septemba ,2017
Wanafunzi
wa Shule za Sekondari za Shirika la Elimu Kibaha wanatarajiwa kuleta mabadiliko
katika ujasiriamali kwa jamii hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la
Elimu Kibaha Bw. Robert Shilingi wakati akizindua rasmi ushirikiano baina ya
Shirika la Elimu Kibaha na Chuo cha Biashara cha Thoren kutoka nchni Sweeden.
Bw.
Robert Shilingi amebainisha kuwa Chuo cha Biashara cha Thoren kimeingia rasmi
katika mashirikiano na Shirika La Elimu Kibaha ambapo wanafunzi wa Shule zote za Sekondari za
Shirikia watapatiwa elimu ya ujasirimali
na biashara ili wamalizapo masomo waweze kuwa chachu ya kuelimisha jamii na hao
wenyewe kushiriki kikamilifu katika
ujasiriamali.
Kwa
upande wake Mratibu wa Mashirikiano hayo kutoka Sweden Bi. Sirpa Rydell amesema
Kuwa Chuo chake kimeingia katika mashirikiano na Shule za Shirika la Elimu
Kibaha ili kuwajengea uwezo wa elimu na mbinu mbalimbali za ujasiriamali ili
kuwawezesha wamalizapo masomo waweze kujiajiri na kujitegemea.
Akielezea
namna mradi huo utawanufaisha wanafunzi Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu
Bw. Chrisdom Ambilikile amesema mashirikiano hayo yanalenga kuwapa uwezo
wanafunzi elimu ya ujasiriamali na kutoa elimu kwa jamii mzima inayoizunguka Shirika kuhusu biashara na namna ya kujiajiri.
Mapema
Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la Elimu Kibaha Mwalimu Mchayano Ngonyani
amesema mradi unalenga kushiriki pamoja na juhudi za Serikali za kutengeneza ajira.
Alibainisha Nchini Tanzania ajira nyingi zinategemewa kupatikana Serikalini
huku nafasi hizo bado ni chache hivyo elimu ya ujasiriamali inaweza kuwa chachu
ya kuwapatia ajira vijana wanaohitimu shule kwa kufanya biashara.
Shirika
la Elimu Kibaha lilianzishwa mwaka 1963 wakati huo ikijulikana kama Tanganyika
Nordic Project na baadaye mwaka 1970 Mradi huo ukakabidhiwa rasmi kwa Tanzania
na kuwa Shirika la Elimu Kibaha.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Bw. Robert Shilingi akizindua rasmi mpango wa wa mashirikiano kati ya Shirika la Elimu Kibaha na Chuo cha Biashara cha Thoren cha nchini Sweden katika ukumbi wa B. Merlin.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari za Shirika la Elimu Kibaha wakiwa na wanafunzi wa kutoka Chuo cha Biashara cha Thoren wakisikiliza kwa makini maada zinazotolewa kuhusu ujasirimali katika ukumbi wa B. Merlin
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii akishukuru wageni kutoka Sweden na Shirika la Elimu Kibaha kwa kuanzisha mpango wa Elimu ya Ujasiriamali katika shule zake amabayo ni chachu ya kuleta maendeleo katika Jamii.
Mwanafunzi kutoka Chuo cha Biashara cha Thoren akimkabidhi zawadi kutoka Sweden Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Bw. Robert Shilingi.
No comments: