SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LAPEWA SIFA ILIYOTUKUKA
SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LAPEWA SIFA
ILIYOTUKUKA
Tarehe
30 Septemba, 2017
Shirika
la Elimu Kibaha ina sifa iliyotukuka hayo yamesemwa leo na Rais mstaafu wa
Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya
Hamsini ya Shule ya Sekondari Kibaha yaliyofanyika katika viwanja vya michezo
vya Shirika la Elimu Kibaha.
Dkt.
Kikwete amepata heshima kubwa ya kuwa mgeni rasmi ikizingatiwa aliwahi kusoma
katika Shule ya Sekondari Kibaha ambapo amewatunuku vyeti na kuwapatia zawadi
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha .
Pia
alipata fursa ya kutembelea katika Bweni la Scandia E. na aliweza kuwaonesha
watu waliokuwa katika msafara mahali alipokuwa analala katika bweni hilo.
Aidha
, Dkt. Kikwete alipata fursa ya kukagua maonesho ya taaluma pamoja na
kushuhudia jinsi Skauti wa Kibaha Sekondari walivyo wakakamavu. Amesifiu juhudi
zinazofanywa na Shirika la Elimu Kibaha za kuhakikisha Kibaha sekondari inakuwa
na hadhi ile ile ya kitaaluma kiasi cha mwaka 2016 kuwa Shule ya kwanza kwa
Shule za Serikali katika mitihani ya kidato cha nne.
Pia
ameagiza katika maktaba ya Shirika la Elimu Kibaha vipatikane vitabu
vitakavyowapa elimu ya ziada wanafunzi na kwamba vitabu vya kawaida vya masomo
viwepo shuleni ambapo kila mwanafunzi ataweza kuvisoma.
Pamoja
na hayo ameahidi kuweka pamoja jitihada zake na za watu aliowahi kusoma nao katika
kuchangia ukarabati wa Shule ya Sekondari ya
Kibaha ambayo imetoa viongozi wengi ambao wapo Serikalini na katika Vyuo
Vikuu mbalimbali nchini Tanzania. Shule ya Sekondari Kibaha kwa sasa ina zaidi
ya miaka hamsini.
No comments: